Katibu mkuu wa muda mrefu wa chama cha waalimu nchini (KNUT) Wilson Sossion amejiuzulu saa chache kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi wa chama hicho.
Akitoa sababu za kujiuzulu kwake, Sossion ameilaumu serikali kwa kuhujumu oparesheni za chama hicho kwa kuwanyima ada zinazotolewa na walimu hali ambayo imewasababisha viongozi wenzake kukosa mshahara kwa muda wa miaka miwili.
Sossion ambaye amekuwa kwenye mapambano na mwajiri wake TSC amesema ataendelea kutekeleza majukumu yake kama mbunge mteule bungeni akishiria kwamba atajiunga na siasa hivi karibuni.