Kaunti ya Baringo imeathirika zaidi na visa vya watu kung’atwa na nyoka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayojumuisha msimu mrefu wa ukosefu wa mvua.
Nyoka hatari wanapatikana katika kaunti hiyo na wamewang’ata wengi ambao wameishia kupoteza maisha au kulemaa kama anavyoeleza mmoja wa wakaazi Jackson Kiplagat kutoka Emsos anasema kwamba wanawe kwa sasa hawawezi tembea mmoja wao akifariki.
Mbali na nyoka,viboko na mamba kutoka ziwa Baringo wameripotiwa kuwavamia wakazi na hivyo kusababisha mzozo baina ya wanyama na wanadamu.
Ni kutokana na hilo ndiposa waziri wa Utalii Najib Balala anasema serikali imezindua mpango wa kuwafidia walioshambuliwa na wanyama ambapo kima cha Sh529M kwa zaidi ya waathiriwa 4000 kitatumika.
Gavana wa Baringo Stanley Kiptis ametoa wito wa kuharakishwa kwa walipo hayo ili wenyeji wapate haki hatimaye.