Milango Yafunguliwa Kwa Waangalizi wa Uchaguzi wa EU 2027.

0

Rais William Ruto ameashiria utayarifu wa Kenya kuwa mwenyeji wa waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 2027.

Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi Mnamo siku ya Alhamisi tarehe 12 Novemba 2026, alipokuwa mwenyeji wa mabalozi 44 wa Umoja wa Ulaya wanaohudumu katika mataifa mbalimbali ya Afrika, Rais Ruto amesema Kenya iko tayari kufanya mashauriano kuhusu ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja huo kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

“Kenya inaendelea kujitolea kuzingatia utawala wa sheria, uwajibikaji na haki za binadamu,” amesema Rais Ruto.

“Tunapojiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 2027, tunakaribisha mashauriano kuhusu ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya, kwa kuzingatia sheria na taratibu zetu.” Ameongeza.

Mkutano huo umefanyika wakati Kenya na Umoja wa Ulaya wanaadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia, huku Rais Ruto akitoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano katika biashara, uwekezaji, usalama na maendeleo.

Rais amesema Umoja wa Ulaya unachangia asilimia 21 ya bidhaa zote zinazouzwa na Kenya katika masoko ya kimataifa, hasa chai, kahawa, mazao ya kilimo cha bustani na maua.

Aidha, ametoa wito kwa wawekezaji wa Ulaya kuongeza uwekezaji katika sekta za viwanda, kilimo, nishati na afya, akisema uwekezaji huo unapaswa kubuni fursa za ajira, na kuimarisha viwanda vya ndani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here