Joho Atakiwa Kujiwasilisha Mbele ya Bunge la Seneti.

0

Bunge la Seneti limemwagiza Waziri wa Madini Hassan Joho kufika mbele yake kufafanua kuhusu agizo lake lenye utata linaloruhusu kuanza tena kwa uvuvi katika ziwa Nakuru

Agizo la Joho ni licha ya onyo la serikali kuwa Samaki katika ziwa hilo wanaweza kuwa hatari kwa matumizi ya binadamu

Kamati ya Seneti ya usalama wa taifa inamtaka Joho kueleza msingi ya kisayansi iliyochangia agizo lake lililoibua mzozo kuhusu uvivu haramu katika hifadhi ya kitaifa ya ziwa Nakuru

Kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Isiolo Fatma Dullo imesema hakikisho la Waziri huyo linapingana na matokeo ya mashirika ya serikali ambayo yameonya mara kwa mara dhidi ya kuvua Samaki katika ziwa hilo

Joho anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Novemba 26 ili kutoa maelezo kuhusu agizo hilo

Agizo la Waziri Joho liliibua maswali kuhusu afya ya umma na uhifadhi na utekelezaji wa vikwazo vya uvuvi

Mzozo huo ulizuka baada ya Joho akizungumza katika hafla ya uwezeshaji huko Nakuru mwezi uliopita kueleza maafisa wa polisi wasiwakamate wavuvi wanaofanya kazi ziwani akisema amewaruhusu kuendelea kuvua Samaki

“Ninawaagiza maafisa wa polisi kuacha kuwasumbua wavuvi katika Ziwa Nakuru. Ninatoa agizo hili katika nafasi yangu kama Waziri wa Madini anayesimamia masuala ya uvuvi. Wavuvi hawapaswi kunyanyaswa na mtu yeyote,” alisema Joho.

Huduma za uvuvi ya Kenya hivi majuzi iliambia kamati ya seneti ya usalama kwamba ziwa Nakuru sio eneo teule la kufanyia uvuvi

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here