Kampeini ya kutoa chanjo dhidi ya ukambi kwa watoto walio na umri wa kati ya miezi tisa hadi miaka mitano kwa kaunti Ishirini na mbili imeanza rasmi hii leo.
Katibu mwandamizi katika wizara ya Afya Dr. Mercy Mwangangi ameanzisha rasmi kampeini hiyo inayowalenga watoto Million 3.5 katika kaunti ya Kajiado
Kampeini hiyo inayogharimu Sh800M inatolewa kufuatia mkurupuko wa ukambi nchini, na haswa katika kaunti za Mandera, Pokot Magharibi, Wajir, Garissa na Tana River.
Kaunti zingine ni; Baringo, Turkana, Elgeyo Marakwet, Busia, Homabay, Migori, Kisii, Kajiado, Nairobi, Bomet, Bungoma, Kakamega, Narok na Vihiga.
Maeneo yatakayolengwa ni sokoni, shuleni, kanisani na kwenye misikiti.