Makachero kutoka idara ya upelelezi (DCI) wamemshika mwalimu anayedaiwa kuwa mshukiwa mkuu wa visa vya wizi wa mtihani wa KCSE katika eneo la Nyanza.
Calvin Magolo, mwalimu wa shule ya upili ya Nyagwethe, Homa Bay anadaiwa kusambaza karatasi feki za mtihani huo katika kaunti za Kisii, Nyamira na Migori kwa mujibu wa kamishna wa kaunti ya Homa Bay Moses Lilan.
Kamishna huyo anasema wanachunguza kujua vipi mshukiwa amekuwa akishirikiana na watu wengine kusambaza karatasi hizo.
Yakijiri hayo
Wizara ya Elimu kwa mara nyingine imewaonya watu wanaosambaza karatasi ghushi za mtihani wa kitaifa wa KCSE unaoendelea.
Katibu katika wizara hiyo Julius Jwan anasema mtihani huo umelindwa vyema na kwamba karatasi zinazosambazwa mitandaoni haswa Whatsapp ni ghushi.
Juan ametoa hakikisho kuwa licha ya mvua kubwa inayosabbaisha mafuriko katika baadhi ya maneo nchini, wamejiandaa vyema na helikopta ambazo zitatumika mahala barabara hazitakuwa zinapitika.