Polisi wa trafiki wako chini ya maagizo kuhakikisha kwamba magari ya uchukuzi wa umma yanazingatia kikamilifu masharti ya kuzuia msambao wa ugonjwa wa corona.
Mratibu wa usalama katika eneo la Nairobi James Kianda anasema watakuwa macho kuhakikisha kuwa hakuna magari yatakayopatikana barabarani baada ya saa mbili usiku na kubeba abiria kuzidi kiasi.
Akizungumza baada ya kukutana na makanda wa Polisi Nairobi, Kianda amesema watafanya kila juhudi kutekeleza marufuku ya kuingia na kutotoka katika kaunti tano zinazoripoti maambukizi ya juu ya corona ikiwemo Nairobi, Machakos, Kaimbu, Nakuru na Kajiado.