Wauguzi wanaogoma wamesema kuwa wataunga mkono mswada wa marekebisho ya katiba BBI iwapo tume ya huduma za afya itarejeshwa kwenye ripoti hiyo.
Wakiongozwa na katibu mkuu wa muungano wa wauguzi KNUN Seth Panyako, wahudumu hao wa afya wamesema tume hiyo ni muhimu kwani itashughulikia maswala yote yanayowahusu.
Panyako vile vile amemkashifu mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya kwa kutishia kuwafuta kazi Wauguzi wanaogoma.
Katibu mkuu wa chama hicho {KNUN} Maurice Opetu anasisisiza kuwa watarejea kazini iwapo magavana watatia sahini mkataba wao wa makubaliano.
Wakati uo huo
Katibu mkuu wa muungano wa kutetea maslahi ya wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli ameomba serikali ya kitaifa kuingilia kati na kumaliza mgomo wa wahudumu wa afya unaoendelea.
Katika kikao na wanahabari, Atwoli ameomba waziri wa afya Mutahi kagwe na waziri wa leba Simon Chelugui kufanya mazungumzo na magavana ili wapate suluhu la kudumu
Atwoli ametetea muungano wa COTU akisema hawajajitenga na mgomo huo unaoendelea na kuwa wamekuwa katika mkutano na waziri Chelugui kutafuta suluhu.
Atwoli amesema kuwatisha na kuwafuta kazi wahudumu wa afya si suluhu.