Mahakama imetoa agizo linalozuia kuapishwa kwa Anne Kananu kama gavana wa Nairobi.
Agizo hilo limetolewa na jaji Anthony Mrima kwenye kesi iliyowasilishwa na chama cha Mawakili nchini LSK.
Kesi hiyo inatazamiwa kusikilizwa Januari 28.
Kananu aliapishwa mapema leo baada ya spika wa bunge la kaunti ya Nairobi Benson Mutura kujiondoa kama kaimu gavana.
Katika kikao na wanahabri katka majengo ya City Hall, Mutura amemtakia kila la kheri mrithi wake ambaye sasa anachukua kutoka kwa aliyekuwa Gavana Mike Sonko aliyetimuliwa.
Kananu amesema ataapishwa kuingia afisini kama gavana wa kaunti ya Nairobi kabla ya kutamatika kwa siku kumi na nne kama ilivyo kikatiba