Bweni la shule moja kaunti ya Narok lateketea

0

Mali ya thamani isiyojulikana imeteketea baada ya bweni la shule ya Oloormirani kaunti ndogo ya narok magharibi kuteketea jana jioni.

Wanafunzi waliokuwa darasani wakati moto huo ulipozuka mwendo was aa moja usiku, walipoteza vitu vyao vya kibinafsi ikiwemo matandiko.

Wazima moto kutoka Narok mjini walifika saa moja baada ya wanafunzi na walimu kwa usaidizi na wanakijiji kufaulu kuuzima moto huo.

Uchunguzi kuhusu mkasa huo unanedelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here