Kenya yaripoti visa vipya 166 vya corona, 262 wapona, 3 wafariki

0

Watu 166 wamepatikana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 98,859.

Katika taarifa iliyotumwa na wizara ya afya, watu 262 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 82,195.

Wagonjwa wengine 3 wameaga dunia na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,726.

Watu 683 wamelazwa hospitalini na wengine 1,726 wanashughulikiwa nyumbani.

Wagonjwa walio katika chumba cha watu mahututi ni i 29.

Maambukizi katika kaunti ni kama yafuatayo Nairobi 115, Kiambu 10, Kajiado 7 na Mombasa 6.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here