Watu 65 wakutwa na corona, 77 wapona, 3 wafariki

0

Watu 65 zaidi wamepatikana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 99,227.

Kupitia kwa taarifa iliyotumwa na wizara ya afya, watu 77 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 82,427, watu wengine 3 wameaga dunia na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,734.

Watu 697 wamelazwa hospitali wengine 1,680 wanashughulikiwa nyumbani huku wagonjwa walio katika chumba cha watu mahututi wakiwa 28.

Maambukizi katika kaunti ni kama ifuatavyo Nairobi 53, Kajiado 3, Mombasa 2, Kitui 2.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here