Watu 604 wakutwa na corona, 10 zaidi wakifariki

0

Watu 604 wameambukizwa virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya kupima sampuli 5,832.

Hii inafikisha 42,541, idadi yavisa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa amesema kuwa idadi ya waliopona ugonjwa huo imefika 31,428 baada ya watu 88 zaidi kupona.

Maafa yanayotokana na ugonjwa huo yamesalia kuwa juu huku watu 10 zaidi wakifariki na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 797.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 125, Nakuru 113, Mombasa 87, Busia 35, Uasin Gishu 33,Trans Nzoia na KIambu 25,Ksii na Kisumu 24, Kajiado 16, Nandi 13, Kakamega 12, Meru 11, Machakos, Siaya na Garissa 7,Muranga ,West pokot,Nyeri 5,Turkana 4, Laikipia, Wajir, Embu, Kirinyaga, Narok, Marsabit na Taita Taveta 2, Kitui, Nyamira, Tharaka Nithi, Kilifi na Nyandarua 1.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here