Bei za mafuta zapungua

0

Bei ya mafuta ya petrol imepanda kwa Sh0.72 kwa kila lita jijini Nairobi huku bei ya mafuta ya diseli ikipungua kwa Sh2.18.

Bei ya mafuta inasalia ilivyo bila kupanda au kupungua katika muda wa siku 30 zijazo kuanzia leo usiku.

Jijini Nairobi, Petroli lita moja itapatikana kwa Sh107.27 huku Diseli ikiuzwa kwa Sh92.91. Mafuta taa yatasalia kuuzwa kwa Sh83.73 kwa kila lita.

Lita moja ya Petroli itapatikana kwa Sh104.86 mjini Mombasa, Diseli Sh90.53 huku mafuta taa yakiuzwa kwa Sh81.37.

Mjini Nakuru, Petroli itauzwa kwa Sh106.96, Diseli kwa Sh92.85 na mafuta taa kwa Sh83.69. Wakaazi wa Eldoret watanunua lita moja ya Petroli kwa Sh107.89, Diseli kwa Sh93.77 na mafuta taa kwa Sh84.61.

Kisumu Petroli lita moja itauzwa kwa Sh107.88, Diseli kwa Sh93.77 huku mafuta taa yakiuzwa kwa Sh84.60.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here