LSK wapata pigo mahakamani

0

Chama cha mawakili nchini LSK kimepata pigo baada ya mahakama kukataa kutoa agizo la muda linalozuia kutekelezwa kwa masharti ya usalama yaliyotolewa na kamati ya kitaifa ya usalama kudhibiti mikutano ya hadhara.

Jaji wa mahakama kuu Antony Murima ambaye amekataa kutoa agizo hilo ametaka pande husika kupewa stakabadhi za kesi hiyo kufikia kesho Octoba 16.

Miongoni mwa maombi ya LSK ilikuwa ni kuondolewa kwa sharti la kuwataka Polisi kutoa kibali kabla ya kuandaliwa kwa mkutano wowote na vile vile maafisa wa usalama kuwa na uwezo wa kupiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote.

Hayo yanajiri huku kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua akiwataka Wakenya kupinga masharti hayo kwa misingi kwamba serikali inatumia sheria hizo za kudhibiti mikusanyiko kuwakandamiza wakosoaji wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here