Wandayi Atetea Ujenzi wa Kiwanda cha Mafuta Tanga, Tanzania.

0

Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi ametetea ujenzi wa kiwanda cha mafuta eneo la Tanga katika nchi jirani ya Tanzania akisema ni uamuzi wa kibiashara.

Akitetea hatua hio Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi amesema Tanga liko katika eneo la kimkakati kwa biashara kati ya mataifa kama Uganda, Tanzania na Kenya ikilinganishwa na Mombasa.

Wandayi alikuwa akijibu maswali kutoka kwa Seneta wa Mombasa Mohammed Faki aliyetaka kujua sababu ya Kenya kuwekeza kwenye kiwanda Tanga wakati ambapo inakodishia raia wa kigeni kiwanda cha Changamwe.

“Kufungwa kwa kiwanda cha Changamwe kulitokana na masuala ya kiuchumi na gharama za uendeshaji, na hilo ndilo lililoelekeza msingi wa mpango wa kuanzisha kiwanda Tanga kitakachohudumia si Kenya pekee bali pia nchi jirani.” Amesema Wandayi.

Wandayi aidha amefafanua kuwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu Kenya itakuwa inazalisha mafuta ghafi.

Hata hivyo, ameeleza kuwa kiwango cha mafuta kinachotarajiwa kutoka Lokichar hakitoshi kuendesha kiwanda cha kusafisha mafuta kwa misingi ya kibiashara.

“Kwa mara ya kwanza, Kenya itaanza uzalishaji wa kibiashara wa mafuta kabla ya mwisho wa mwaka huu.” Amesema.

“Viwango vinavyotarajiwa kutolewa kutoka Lokichar havitaweza kusambaza mafuta hitajika kuendesha kiwanda cha mafuta.

Waziri huyo amesema Kenya itazalisha kati ya pipa elfu ishirini na hamsini ya mafuta ghafi ikilinganishwa na hitaji ya mapipa laki tano inayohitajika kuendesha kiwanda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here