Wanafunzi wa shule ya wasichana ya Lugulu kaunti ya Bungoma wameandamana leo kulalamikia mmoja wao kudhulumiwa kimapenzi.
Masomo yamesitishwa shuleni humo baada ya wanafunzi kuandamana barabarani.
Wanafunzi waliandamana hadi katika kituo cha Polisi cha Webuye kushinikiza kukamatwa kwa aliyehusika na kitendo hicho.
Walibeba mabango wakiimba nyimbo za kutaka haki ikitendeke kwa mwenzao.
Mwanafunzi huo anaarifiwa kubakwa Jumamosi asubuhi aliokuwa anaoga kabla ya kuelekea darasani.
Aliokolewa na mwenzake aliyefika kwa ghafla na kuanza kupiga kamsa na kumlazimu mshukiwa kutoroka.