Ruto ataka maslahi ya wahudumu wa afya ipewe kipau mbele

0

Naibu rais William Ruto ametaka maslahi ya wahudumu wa afya kupewa kipau mbele wakati huu taifa linakumbwa na mgogoro wa kiafya.

Akizungumza wakati wa mazishi ya Jenerali mstaafu John Koech katika eneo bunge la Ainamoi kaunti ya Kericho, Ruto amesema mipango yote inafaa kuwekwa kando angalau kwa sasa ili kuangazia kilio chao.

Naibu rais ambaye pia amewashauri Wakenya kuendelea kuzingatia masharti ya usalama amesema wizara ya afya imeagizwa kushiriki kwenye mazungumzo na wawakilishi wa miungano hiyo ya afya kwa lengo la kutafuta suluhu la kudumu.

Wakati uo huo katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi amewarai wahudumu wa afya wanaogoma kusitisha mgomo wao serikali inaposhughulikia malalamishi yao.

Haya yanajiri huku wahudumu wa afya wakiwemo wauguzi na matatibu wagoma kulalamikia maswala mbalimbali ikiwemo kupewa vifaa vya kujikinga PPEs pamoja na bima ya matibabu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here