Wakaazi wa Kilifi waonywa dhidi ya kula nzige

0

Gavana wa Kilifi Amason Kingi amewaonya wakaazi wa kaunti hiyo dhidi ya kukula nzige wa jangwani.

Kingi anasema huenda baadhi ya nzige hao wako na kemikali waliyomuagiwa hapo awali kwa hivyo kuwafanya kuwa hatari.

Onyo hilo linajiri huku baadhi ya wenyeji wakifanya nzige waliovamia kaunti hiyo kuwa kitoweo wakisema ni chakula kitamu.

Hata hivyo gavana Kingi ametoa hakikisho kwamba serikali yake inafanya kila juhudi kudhibiti hali kuzuia kuenea kwa wadudu hao kabla ya kusababisha hasara kwa mimea.

Wauguzi pamoja na matabibu wanakutana katika bustani ya Uhuru Park kwa hafla ya maombi ya kuwakumbuka wenzao ambao wamepoteza maisha kutokana na janga la COVID19.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here