Wanafunzi wa mwaka wa mwisho kuripoti shuleni Jumatatu ijayo

0

Wanafunzi wa mwaka wa mwisho katika vyuo vikuu sawa na taasisi za kutoa mafunzo ya kiufundi (TVETS) wametakiwa kuripoti shuleni Jumatatu ijayo ambayo ni Octoba 5 huku serikali ikilenga kufungua tena taasisi za masomo kwa awamu.

Waziri wa elimu Profesa George Magoha katika taarifa amesema vyuo hivyo vitatoa tarehe ya kurejelewa kwa masomo ila kwa kuzingatia masharti ya wizara ya afya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Kabla ya kuruhusiwa kufunguliwa kwa minajili ya kuendelea na masomo, waziri Magoha amesema ni sharti maagizo ya usalama ya wizara ya afya yafuatwe kikamilifu.

Bodi simamizi za vyuo hivyo zimetakiwa kuhakikisha kuwa masharti hayo yamezingatiwa kabla ya vyuo hivyo kufunguliwa huku maafisa wa elimu wakiagizwa kuhakikisha kuwa maagizo hayo yamefuatwa.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here