Wakenya wamepoteza takribani shilingi bilioni 2.3 katika mamlaka ya kusambaza dawa na vifaa vya matibabu nchini (KEMSA)
Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyowasilishwa mbele ya kamati maalum ya bunge la seneti na mkaguzi mkuu wa hesabu za umma Nancy Gathungu.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa maafisa wakuu wa KEMSA walikiuka sheria za ununuzi wa vifaa vya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona na kusababisha kupotea kwa pesa za mlipa ushuru.
Gathungu anasema maafisa hao waliongeza bei ya vifaa walivyonunua kwa tarkibani shilingi bilioni 6.3 kwani endapo vitauzwa sasa watapata hasara ya shilingi bilioni 2.3.
Ripoti hiyo imefichua udanganyifu uliofanywa na maafisa wakuu wa KEMSA kwa ushirikiano na kampuni ambazo zilizopewa kandarasi mbalimbali za mabilioni ya pesa.