Wakenya wataambiwa kupitia ujumbe mfupi kuhusu ni lini na wapi watapata kadi zao za Huduma Namba hivi karibuni.
Kupitia taarifa, wizara ya mambo ya ndani imesema waliojiandakisha kupata kadi hizo watafahamishwa kupitia SMS kuhusu ni vipi watapata kadi zao.
Wizara hiyo inasema shughuli ya kuchapisha kadi hizo inaendelea na zoezi la kuanza kuwapa wale waliosajiliwa litaanza hivi karibuni.
Serikali imeashiria kwamba matumizi wa vitumbulisho vya kitaifa yanatazamiwa kufikia kikomo Disemba 12 mwaka huu.
Rais Uhuru Kenyatta pamoja na mkewe Margaret Kenyatta ndio walikuwa wa kwanza kupata kadi hizo Octoba 20 mwaka jana wakati wa sherehe za Mashujaa katika kaunti ya Kisii.