Magoha awalaumu wazazi kufuatia kuongezeka kwa visa vya utundu miongoni mwa wanafunzi

0

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amewalaumu wazazi kutokana na kuongezeka kwa visa vya wanafunzi kuwashambulia walimu.

Profesa Magoha amesema wazazi wamekuwa wakiwabembeleza watoto wao kama mayai wakati ule shule zilikuwa zimefungwa kwa sababu ya janga la corona na hivyo kuwafanya kuwa watundu.

Kutokana hilo, waziri Magoha amezitaka asasi husika kuwachukulia hatua kali wanafunzi wanaotekeleza uhuni huo na kutoa wito kwa walimu kuhakikisha kuwa wanajilinda.

Kauli za Magoha zinawadia wiki moja baada ya walimu wawili kushambuliwa katika kaunti za Kisii na Nyamira na wanafunzi waliojihami.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here