Donald Trump ameondoka katika Ikulu ya White House kwa mara ya mwisho na kutoa nafasi ya kuapishwa kwa mrithi wake Joe Biden.
Trump ni rais anayeondoka kususia hafla ya kuapishwa kwa mrithi wake ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo.
Katika hotuba yake ya mwisho, Trump amewapongeza Marekani kwa kumpa fursa ya kuwaongoza na kumtakia Biden na uongozi wake kila la kheri.
Mwanasiasa huyo amekuwa akisisitiza kuwa uchaguzi wa Marekani mwaka jana haukuwa huru na haki ambapo zaidi ya mara moja amekuwa akidai kwamba kura zake ziliibiwa.