Miili ya watu sita wasiojulikana imepatikana na majeraha ya risasi kichwani katika eneo la Arabal huko Baringo Kusini.
Kiini cha mauji hayo hakijabainika ila yamehusishwa na wizi wa mifugo ambao umekuwa ukishuhudiwa katika baadhi ya sehemu za Baringo.
Maafisa wa polisi wamemepeleka miili hiyo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Baringo.
Kiini cha mauji hayo hakijabainika ila yamehusishwa na wizi wa mifugo ambao umekuwa ukishuhudiwa katika baadhi ya sehemu za Baringo.
Yanajiri haya wakati ambapo oparesheni inaendelea kuwaondoa wahalifu wanaodaiwa kuhusika na misururu ya visa vya utovu wa usalama katika eneo la Kapedo.
Hata hivyo baadhi ya viongozi kutoka Baringo na Pokot wamepinga oparesheni hiyo ya kiusalama wakisema matumizi ya nguvu kupita kiasi sio suluhu.
Wakiongozwa mbunge wa TiatyWilliam Kamket, viongozi hao wameitaka serikali kubadili mbinu ya kutafuta suluhu ya visa vya hivyo vya utovu wa usalama kupitia kufanya uchunguzi na kubaini kiini halisi.
Naye kiongozi wa walio wengi katika bunge la Senate Samwel Poghisio amesema oparesheni hiyo inafaa kusitishwa kwa sababu raia wasiokuwa na hatia wanaendelea kuumizwa na maafisa wa usalama.
Oparesheni hiyo imeanzishwa baada ya kuuawa kwa afisa mmoja wa GSU na wenzake wawili sawa na wizi wa mifugo ambao umeendelea kusababisha hofu miongoni mwa wenyeji.