Maafisa wengine wawili wa polisi wauwawa Kapedo

0

Chifu inspekta wa polisi na dereva wake ambaye pia ni afisa wa polisi wameuwawa na washukiwa wa wizi wa mifugo katika kivukio cha Kapedo.

Mkuu wa polisi katika eneo hilo George Natembeya anasema wawili hao na raia mmoja walikuwa wanatoka hafla ya mazsihi kabla ya kufumaniwa na wahalifu hao wakirejea kambini.

Inaripotiwa wawili hao walienda mbele ya msafara wa magari uliokuwa unatoa ulinzi kabla ya kukumbana na mauti yao.

Wakaazi wa eneo hilo wanaioma serikali kuimarisha usalama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here