Wanaotaka kuwania urais kwa tiketi ya chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga watakuwa na fursa ya kuwasilisha maombi yao katika muda wa siku tatu zijazo
Katibu mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna amesema uamuzi huu umeafikiwa kwenye mkutano wa kamati ya uongozi ya chama hicho ulioandaliwa leo katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2022.
Mbali na kumtafuta muwaniaji wake wa urais kwenye uchaguzi huo, chama hicho kinatazamiwa kuandaa chaguzi za mashinani kote nchini huku ratiba ikitazamiwa kutolewa chini ya siku saba zijazo.
Kuhusu ushirikiano na mirengo mingine ya kisiasa, kamati hiyo ya uongozi imeafikia kuwa mazungumzo yoyote na vyama vingine ni sharti yawe rasmi.
Chama hicho cha ODM aidha kimesema kitamteua naibu gavana katika kaunti ya Nairobi huku kikipendekeza jina la mtu mwingine kuwa naibu gavana katika kaunti ya Nyamira baada ya bunge la kaunti hiyo kumkataa James Gesami.