Mahakama ya Milimani inayoshughulikia kesi za kifamilia imefungwa kwa muda wa siku 7 baada ya wafanyikazi watatu kukutwa na corona.
Akitoa tangazo hilo, kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu amearifu kwamba mmoja wa wafanyikazi hao amelazwa hospitalini.
Mwilu ameeleza kuwa mahakama hiyo huwa na shughuli nyingi kila siku huku wafanyikazi pamoja na watu wa kawaida wakitangamana na hivyo kuwepo kwa haja ya kufungwa kwa muda.
Kufungwa kwa mahakama hiyo kutatoa nafasi ya wafanyikazi wake kujitenga kuzuia maambukizi zaidi kuambatana na taratibu za wizara ya afya.