Odinga yuko katika hali nzuri adhibitisha daktari wake

0

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameshauriwa kupumzika baada ya kufanyiwa vipimo vya matibabu katika hospitali ya Nairobi.

Daktari wake David Oluoch Olunya amedhibitisha kuwa waziri huyo mkuu wa zamani yuko katika hali nzuri ya kiafya ila anaendelea kumfuatilia kwa karibu baada ya vipimo hivyo.

Amesema Odinga alifika katika hospitali Jumanne kukaguliwa baada ya kuhisi uchovu.

Daktari huyo amesema Odinga anaendelea kutizamwa na kundi la wataalamu na mengi zaidi kuhusu afya yatatolewa baada ya uchunguzi.

Nduguye mkubwa Oburu Odinga ametoa hakikisho kuwa hali ya kiafya ya kakake ni shwari na kwamba hamna cha kuhofia.

Odinga hakuonekana hadharani wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya handisheki ambapo aliratibiwa kufanya kikao na Rais Uhuru Kenyatta katika ikulu ya Rais.

Itakumbukwa kwamba kiongozi huyo wa chama cha ODM amekuwa katika misururu ya mikutano ya kisiasa wiki nzima katika eneo la Pwani kupigia debe mswada wa marekebisho ya katiba BBI.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here