Aliyekuwa rais wa Somalia Ali Mahdi Muhammad, 82, amefariki akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi.
Taarifa kuhusu kifo chake imedhibitishwa na msemaji wa wizara ya Mawasiliano ya Somalia Ismael Mukhtaar Omar.
Omar hajatoa maelezo zaidi kuhusu kifo hicho ila ripoti zaarifu kuwa rais huyo wa zamani alikuwa amelazwa kwa muda wa siku tatu.
Muhammad alikuwa rais wa Somalia kuanzia Januari 1991 hadi January 1997 baada ya kumpindua Mohamed Siad Barre aliyekuwa ameongoza kimabavu kuanzia Octoba mwaka 1969.
Alihudumu kama rais hadi kuchaguliwa kwa Abdiqasim Salad mwaka 2000.









