Wafanyikazi KNH watoa makataa ya siku saba kugoma

0

Wahudumu wa afya katika hospitali kuu ya kitaifa ya Kenyatta (KNH) wametishia kugoma kuanzia Jumatatu wiki ijayo iwapo mkataba wa maelewano wa 2012 hautatekelezwa.

Wakiongozwa na katibu mkuu wa muungano wa madaktari (KMPDU) tawi la Nairobi Thuranira Kaugiria, wahudumu hao wakiwemo madaktari na wauguzi wametoa makataa ya siku saba kwa serikali iwalipe mishahara na marupuru yao ilivyo kwenye mkataba huo la sivyo wagome.

Katibu mkuu wa muungano wa Wauguzi (KNUN) Seth Panyako ameshutumu tume ya kuratibu mishahara ya watumishi wa umma (SRC) kwa kuiandikia hospitali ya Kenyatta isiwalipe mishahara yao huku wakitishia kuandamana hadi katika makao makuu ya tume hiyo jijini Nairobi.

Mgomo huu huu unajiri wakati ambapo kaunti mbalimbali zinashuhudia migomo wa wahudumu wa afya kulalamikia kutolipwa licha ya taifa kuendelea kupambana na janga la COVID19.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here