Walimu wana hadi Jumatatu kurejea shuleni

0

Tume ya huduma za waalimu (TSC) imewataka Waalimu kurejea shuleni kufikia Jumatatu ijayo tarehe 28 mwezi huu ili kujiandaa kwa ufunguzi wa shule.

Afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia anasema walimu wako tayari kuhakikisha kuwa wanafunzi wanamaliza mwaka huu wa masomo ambao umesambaratishwa kwa zaidi ya miezi sita sasa.

Haya yanajiri huku serikali ikiongeza muda kwa wahudumu wa Juacali kutengeneza madawati ya shule hadi Ijumaa wiki hii.

Shule za msingi zitapata madawati 70 huku zile za upili zikipata madawati 50 kila moja.

Wakati uo huo…

Washikadau wa elimu wamekubaliana kuhusu tarehe ya ufunguzi wa shule na ratiba ya masomo iliyosambaratishwa na janga la COVID19.

Akizungumza baada ya kupokea ripoti kuhusu ufunguzi wa shule, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema watawasilisha ripoti hiyo kwa kamati kuu ambayo itajadaili kufunguliwa kwa uchumi baadae wiki hii.

Magoha pia amesema kuwa wanafunzi wa chuo kikuu wa masomo ya sayansi ambao hawajakamilisha mitihani yao ya mwisho wanaweza kurejea shuleleni ili kukamilisha.

Magoha ameongeza kuwa shule ambazo zimeharibiwaau kukosa miundo msingi inayofaa, wanafunzi watahamishiwa hadi shule zingine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here