Wabunge wawili wapigana kwenye mazishi

0

Kumekuwa na hali ya vuta nikuvue katika mazishi ya babake naibu gavana wa Kisii Joash Mangi wakati mbunge wa Mugirango Kusini Silvanus Osoro walipokabiliana kwa makonde na mwenzake wa Dagoreti Kaskazini Simba Arati.

Makabiliano hayo yalijiri wakati Osoro aliinuka kwa hasira alikokuwa ameketi na kuelekea jukwani kujaribu kumnyang’anya kipaza sauti mwenzake Arati kwa kumkosea heshima naibu rais William Ruto.

Iliwalazimu maafisa wa usalama na viongozi wengine kuiingilia kati na kutuliza vurugu hizo ambazo nusra zikatize mazishi hayo.

Naibu rais William Ruto na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga walihudhuria mazisho huku siasa za BBI zikitawala.

Wakati huo

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi amewasihi Wakenya kuwaombea viongozi na amani katika taifa hili kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza mjini Eldoret Sudi amewataka Wakenya kujitenga na siasa za ukabila na badala yake kukumbatia uwiana na utangamano wa taifa.

INSERT: SUDI ON AMANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here