Simon Nyache aaga dunia

0

Aliyekuwa waziri mwenye ushawishi mkubwa Simeon Nyachae amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Mwanawe Charles Nyachae amesema marehemu amefariki akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi.

Nyachae alihudumu kama mbunge wa Nyaribari Chache kuanzia mwaka 1992 alipochaguliwa kuwa waziri wa Kilimo na kisha akahamishwa hadi katika wizara ya Fedha.

Aliwakilisha eneo bunge la Nyaribari Chache kwa miaka 15 kabla ya kushindwa na Robert Monda mwaka 2007.

Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i amewataka Wakenya kuiombea familia ya Nyachae.

Katika uongozi wa rais mstaafu Mwai Kibaki, marehemu Nyachae alihudumu kama waziri wa barabara.

Baadaye alijiuzulu kutoka baraza la mawaziri mwaka 1999 baada ya kuripotiwa kutofautiana na rais mstaafu Daniel Moi.

Nyachae aliwania urais mwaka 2002 kwa tiketi ya chama cha FORD PEOPLE na kuibuka wa tatu baada ya rais Kibaki na Uhuru Kenyatta.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here