Wabunge sugu wa uchochezi watajwa

0

Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC imechapisha majina ya wanasiasa wanne sugu wa kueneza semi za chuki zinazolenga kuligawanya taifa.

Mwenyekiti wa tume hiyo Samuel Kobia amesema wanasiasa hao ni aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko, Mbunge wa Emurua Dikir Johana Ngeno na wabunge waliopigana katika hafla ya mazishi kaunti ya Kisii Simba Arati wa Dagoretti Kaskazini na Sylvanus Osoro Mugirango Kusini.

Kobia amesema viongozi ambao majina yao yatachapishwa mara tatu kwa kutoa matamshi ya uchochezi, watapigwa marufuku kushikilia afisi yeyote ya umma.

Kwa upande mwingine, tume hiyo imewapongeza wabunge Mohammed Abdikahim Osman wa Fafi na Charity Kathambi wa Njoro kwa juhudi zao za kuleta utangamano miongoni mwa jamii mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here