Aliyekuwa waziri na mbunge wa Nyaribari Chache marehemu Simeon Nyachae atazikwa Jumatatu ya tarehe 15, Februari, 2021 nyumbani kwake Kegati kaunti ya Kisii.
Kamati inayoandaa mazishi hayo kwa ushirikiano na familia imesema ibada ya mazishi itafanyika siku hiyo katika uwanja wa michezo wa Nyaturago kabla ya marehemu kuzikwa katika hafla ambayo itahudhuria na familia na watu wachache.
Ibada nyingine ya mazishi itaandaliwa Alhamisi wiki ijayo katika kanisa la kisabato la Nairobi Central – Maxwell.
Nyachae alifariki siku ya Jumatatu wiki hii baada ya kuugua kwa muda mrefu.