Naibu Rais William Ruto Alhamisi hii anaanza ziara ya siku tatu katika kaunti mbalimbali za Pwani kwa mikutano ya kisiasa.
Dr Ruto anatazamiwa kuanzia ziara yake eneo bunge la Lungalunga kaunti ya Kwale ambapo atalakiwa na mbunge Khatib Mwashetani.
Wakati wa ziara hyo, Dr Ruto atazindua miradi mbalimbali iliyofadhiliwa na hazina ya ustawi wa maeneo bunge CDF.
Ijumaa, Naibu Rais atakuwa kaunti ya Mombasa ambapo ameratibiwa kuongoza mchango kwa faida ya makundi ya vijana katika uwanja wa Kadongo kule Kisauni.
Baadaye, ataelekea mjini Frere ambapo ataongoza uzinduzi wa shule ya msingi na ile ya upili ya Kwa Bullo kabla ya kufanya mkutano na wahudumu wa bodaboda.
Ruto anatazamiwa kutumia ziara hiyo kuendeleza siasa zake za hasla, na kupinga mswada wa BBI ambao anasema hauna manufaa kwa mkenya wa chini.









