Afisi kuu ya kanisa la AIC yamuomboleza askofu Nguyo

0

Afisi kuu ya kanisa la Africa Inland, AIC Kenya imetoa rambirambi zake kufuatia kifo cha askofu wa kanisa hilo Dr Benard Nguyo.

Ujumbe maalum ulioongozwa na Askofu Mkuu Abraham Mulwa umetembelea familia hiyo kuipa faraja nyumbani mwa marehemu eneo la Mitaboni kaunti ya Machakos.

Askofu Mulwa aliyeandamana na naibu askofu mkuu Paul Kirui alihimiza familia hiyo wasiwe na hofu na badala yake kuendelea kumtumaini Mungu, akirejelea kitabu cha Yohana 14:1-6.

Wengine ambao waliandamana na Askofu Mulwa kutoa pole kwa familia kutoka afisi kuu ya AIC ni Kasisi John Kitala, mwenyekiti wa bodi ya shirika la habari la Biblia Husema Broadcasting Paul Manyara miongoni mwa wengine.

Kituo cha BHB ambacho marehemu Dr Nguyo amekuwa mwenyekiti wa bodi yake kwa takribani miaka 14 kiliwakilishwa na mkurugenzi mkuu Luka Sawe, wachungaji Festus Kimuyu, Boniface Thenge miongoni mwa wengine.

Marehemu Nguyo atazikwa siku ya Jumatano wiki ijayo, tarehe 10 Februari, nyumbani kwake Mitaboni, kaunti ndogo ya Kathiani, kaunti ya Machakos.

Askofu Mulwa ametoa onyo kwa wanasiasa dhidi ya kuleta siasa haswa za vurugu wakati wa mazishi hayo.

Dkt. Nguyo ambaye hadi kifo chake, alikuwa mmoja wa wakurugenzi wa bodi ya BHB alifariki siku ya Jumapili baada ya kuugua kwa muda mrefu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here