Rais Uhuru Kenyatta amewasihi viongozi kuwa na heshima na waache matusi hata wanapoendeleza azma yao ya kuwania nafasi za uongozi.
Akizungumza katika hafla ya ukumbusho wa rais mstaafu marehemu Daniel Arap Moi, rais Kenyatta amesema taifa hili linafaa kusonga mbele likiwa na umoja na wala sio kubomolewa na viongozi wachache.
Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka akizungumza katika hafla hiyo amemuonya naibu rais William Ruto dhidi ya kuendeleza siasa za matabaka akisema ni hatari kwa taifa hili.
Viongozi mbalimbali walihudhuria hafla hiyo akiwemo kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi, mwenzake wa FORD K Moses Wetangula na katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli.