Bunge la kitaifa limefanyia mabadiliko kalenda yake ikiwemo kuondoa vikao vya siku ya Jumatano kuanzia wiki ijayo.
Kwenye mabadiliko hayo, kutakuwa na vikao viwili kila siku ya Jumanne kikao cha kwanza kikiandaliwa saa nane na nusu mchana hadi saa kumi na mbili na nusu jioni.
Wabunge kisha watakuwa na muda wa dakika thelathini za mapumziko kabla ya kurejelea vikao hivyo kuanzia saa moja hadi saa tatu usiku.
Vikao vya kila Alhamisi vitaanza saa nne asubuhi na kukamilika saa saba za mchana kabla ya kurejea tena kuanzia saa nane na nusu hadi saa kumi na mbili na nusu za jioni. Sawa na ilivyo siku ya Jumanne, wabunge pia watapumzika kwa muda wa dakika thelathini na kurejea tena kuanzia saa moja hadi saa tatu usiku.