Lusaka aidhinisha uamuzi wa kumtimua Kang’ata

0

Spika wa bunge la Senate Ken Lusaka ameridhia uamuzi wa kumuondoa seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata kwenye wadhifa wa kiranja wa wengi katika bunge hilo.

Lusaka kwenye ujumbe wake amesema amepokea uamuzi huo na kwamba ameridhishwa kwamba ulifuata utaratibu wa kisheria.

Kang’ata alifurushwa kwenye wadhifa huo na nafasi yake kutwaliwa na mwenzake wa Kiambu Kimani Wamatang’i kwa misingi kwamba alimkosea heshima kiongozi wa chama cha Jubilee rais Uhuru Kenyatta.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here