Awamu ya pili ya Huduma Namba kuanza Mei

0

Awamu ya pili ya usajili wa watu kupata Huduma Namba itaanza mapema mwezi Mei mwaka huu amesema msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna.

Oguna akiwahutubia waandishi wa habari amesema usajili huo hautafanyika mara moja badala yake utaendelea sawa na inavyofanyika katika kutafuta kitambulisho cha kitaifa.

Amesema awamu ya kwanza ilishuhudia watu milioni 37 wakisajiliwa na kwamba watafahamishwa kuhusu namna watapata kadi zao kupitia kwa ujumbe mfupi.

Msemaji wa serikali vile vile amewataka wale ambao tayari wametumiwa ujumbe huo wachukue kadi hizo ili kupunguza mrundiko.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here