Aliyekuwa askofu wa kanisa la Afrika Inland AIC eneo la Machakos Dkt. Benard Nguyo amezikwa hii leo nyumbani kwake Mitaboni, kaunti ya Machakos.
Kabla ya kumpumzisha marehemu, jamaa, ndugu na marafiki walikongamana katika shule ya upili ya Mitaboni kwenye ibada iliyoongozwa na askofu mkuu wa kanisa la AIC Kenya Abraham Mulwa.
Mkurugenzi wa kituo hiki cha Biblia Husema Broadcasting Lucas Sawe alihudhuria mazishi hayo ikizingatiwa kwamba Dkt. Nguyo hadi kifo chake alikuwa mmoja wa wakurugenzi wa bodi ya BHB.
Waliohudhuria hafla hiyo walimtaja Dkt. Nguyo kama mtumishi alijitolea katika kufanya kazi ya kulihubiri neno lake Mungu.
Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua, seneta wa zamani wa Machakos Johnson Muthama ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo.









