Jopo la kutatua mizozo katika vyama vya kisiasa limebatilisha uamuzi wa chama tawala cha Jubilee kuwafukuza chamani maseneta sita wa kuteuliwa akiwemo Isaac Mwaura na Milicent Omanga.
Mwenyekiti wa jopo hilo Desma Nungo vile vile ametoa agizo linalomzuia msajili wa vyama vya kisiasa dhidi ya kuondoa majina ya maseneta hao kwenye sajili ya Jubilee hadi kesi yao itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Kesi hiyo itasikilizwa Februari 16 na 17.
Maseneta wengine waliokuwa wamefukuzwa chamani ni Mary Yiane, Waqo Jilo, Prengei Victor, Iman Dekow na Christine Zawadi.