Watu 13 watuma maombi kujaza nafasi ya Jaji Mkuu

0

Watu kumi na watatu wakiwemo majaji na mawakili wametuma maombi yao kutaka kujaza nafasi ya jaji mkuu kufuatia kustaafu kwa David Maraga.

Hata hivyo hakuna jaji hata mmoja wa mahakama ya upeo ikiwemo kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu ametuma maombi yake kutaka kumrithi aliyekuwa mkubwa wao.

Miongoni mwa waliotuma maombi yao ni Rais wa mahakama ya Rufaa William Ouko, jaji wa mahakama hiyo Martha Koome, jaji Said Juma Chitembwe na Nduma Nderi wa mahakama kuu na jaji Gitonga Marete wa mahakama ya leba.

Mawakili Fred Ngatia na Philip Murgor ni miongoni mwa waliotuma maombi yao kabla ya kutamatika kwa muda wa kutuma maombi yao Jumanne saa kumi na moja jioni.

Wengine waliotuma maombi yao ni Profesa Patricia Mbote, Profesa Dr Moni Wekesa, Otondi Ontweka, Brian Ombongi Matagaro, Alice Yano na Profesa Otinga Mare.

Tume ya huduma za mahakama JSC sasa ina muda wa majuma mawili kupitia maombi hayo kabla ya kuorodheshwa wale ambao wataitwa kwa mahojiano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here