Muungano wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET sasa unaitaka serikali kuajiri maafisa wa kuwapa adhabu ya kiboko wanafunzi katika kila shule nchini.
Katibu wa muungano huo tawi la Kisumu Zablon Awange anasema walimu hawako tayari kutumia kiboko kwa wanafunzi kwani anadai huenda hilo likazua uhasama baina yao.
Awange anasema pia kuwa serikali imewafuta kazi walimu kadhaa kwa kuwaadhibu wanafunzi na hakuna mwalimu ambaye yuko tayari kupoteza kazi yake tena kwa sababu sawia na hiyo.
Pendekezo la kurejeshwa kwa adhbau ya kiboko shuleni liliafikiwa kufuatia utundu ambao umekuwa ukishuhudiwa miongoni mwa wanafunzi ambao baadhi wanawavamia walimu wakitumia silaha na wengine hata kuchoma shule zao.