Ibada ya wafu kwa mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa waziri Simeon Nyachae imefanyika hii leo katika kanisa la kisabato la Nairobi Central, Maxwell.
Mwanahabari wetu Purity Muema anasimulia zaidi.
Wakizungumza katika kanisa la kisabato la Nairobi Central, Maxwell aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga, mawaziri Dr. Fred Matiang’i wa usalama, mwenzake wa afya Mutahi Kagwe na aliyesoma hotuba ya rais pamoja na kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi wamemtaja Nyachae kama mtu mwenye roho safi
Watoto wake pia akiwemo Charles Nyachae wamemtaja Mzee Nyachae kama baba mkarimu ambaye alikuwa na moyo wa kusaidia.
Nyachae atazikwa Jumatatu ijayo nyumbani kwake Nyosia, Kegati kaunti ya Kisii huku ibada ya mazishi ikiratibiwa kufanyika katika uwanja wa michezo wa Nyaturago.
Nyachae alifariki tarehe moja mwezi huu akiwa na umri wa miaka 88 baada ya kuugua kwa muda mrefu.