Waalimu wameanza kupata chanjo ya corona huku wizara ya afya ikiwalenga zaidi ya walimu 200,000.
Akiongoza uzinduzi wa chanjo hiyo, mwenyekiti wa jopo la COVID19 Willis Akhwale amesema walimu wamepewa kipau mbele kupata chanjo hiyo kwa sababu ya kazi wanayofanya.
Ameongeza kuwa waalimu walio na umri wa miaka hamsini na zaidi ndio watapewa kipau mbele huku akiwashauri walio na magonjwa mengine kuwafahamisha wahudumu wa afya kabla ya kupewa chanjo hiyo.
Yanajiri haya siku moja baada ya Inspekta mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai pamoja na katibu mkuu katika wizara ya usalama wa ndani Dkt.Karanja Kibicho kupewa chanjo hiyo ya corona.
Wawili hao wamewaongoza maafisa wa usalama kupata chanjo hiyo baada ya wahudumu wa afya kuwa wa kwanza kuchanjwa.