Vijana waliotaka kutibua mkutano wa Odinga Githurai watimuliwa

0

Polisi wamelazimika kutumia vitoa machozi kulitawanya kundi la vijana lililojaribu kutatiza mkutano wa kinara wa chama cha ODM Raila Odinga Githurai.

Kundi hilo la vijana lilikuwa linaimba nyimbo za kumsifu naibu rais William Ruto ila juhudi zao kukatiza mkutano wa Odinga zilitibuliwa na maafisa wa Polisi waliokuwa wamejihami.

Odinga amepigia debe ripoti ya BBI akisema kupitishwa kwake kutakuwa na manufaa makubwa kwa Wakenya wote kupitia kuwapa nafasi za kujiendeleza.

Waziri huyo mkuu wa zamani vile vile ameinyoshea kidole cha lawama serikali ya Jubilee kwa kushindwa kutekeleza ahadi ilizotoa kwa Wakenya kipindi cha kampeini za uchaguzi mkuu wa 2013.

Waziri huyo mkuu wa zamani anapigia debe BBI siku moja baada ya tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuidhinisha sahihi zaidi ya milioni moja na kutuma mswada huo kwa mabunge ya kaunti kujadiliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here