Hakimu mkuu Everlyne Olwande ameapishwa kama kamishnna katika tume ya idara ya mahakama JSC.
Hafla ya kumuapisha imeongozwa na kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu katika mahakama ya upeo jijini Nairobi.
Hakimu huyo wa mahakama ya Limuru alichaguliwa Disemba mwaka jana kuwaakilisha majaji na mahakimu katika tume hiyo ya JSC.